“Siku moja naitwa nyota, siku nyingine nakuwa tishio” Amanda Gorman

Haya ndiyo maneno ya mshairi huyo wa hadhi ya juu nchini Marekani baada ya kuhusika katika kioja na afisa wa usalama ijumaa usiki kulingana na saa za Marekani wakati alikuwa akitembea kuelekea kwenye nyumba yake.

Amanda ndiye alijulikanisha haya kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii ambapo aliandika “Afisa wa usalama aliniandama nikielekea nyumbani usiku huu. Alitaka kujua ikiwa ninaishi hapa kwani alinishuku. Nilimwonyesha funguo za nyumba na nikafungua na kuingia ndipo akaondoka, bila kuomba msamaha! Haya ndiyo wasichana weusi wanapitia. Siku moja wanakurejelea kama nyota, siku nyingine unaitwa tishio!”

Dakika chache baadaye mwanadada huyo aliandika tena kwenye mitandao ya kijamii akikiri kwamba yeye ni tishio, aliandika, “Kwa kiwango fulani alisema ukweli. Mimi ni tishio: tishio kwa udhalimu, tishio kwa ukosefu wa usawa, tishio kwa ukosefu wa ufahamu. Yeyote ambaye husema ukweli na kutembea akiwa na wingi wa matumaini ni tishio kwa nguvu fulani.”

Maneno ya binti huyo wa umri wa miaka 22 ambaye ni mkazi asilia wa eneo la Los Angeles, California yalisambaa haraka kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi walionekana kumhurumia.

Mwanahabari wa Ikulu ya White House Yamiche Alcindor alisema kwamba alichokipitia Amanda Gorman ndicho wanachopitia wamarekani wengi weusi na anafurahia kwamba aliweza kufika nyumbani akiwa sawa kwani wengi huwa hawafiki!

Yamiche Alcindor

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *