Siamini Beyonce ni rafiki yangu sasa, Megan Thee Stallion

Mwanamuziki wa Marekani Megan the Stallion haamini kwamba Beyonce ambaye alikuwa akimtazamia siku za awali sasa ni rafiki yake hata na mume wake Jay Z.

Akihojiwa na Stephen Colbert kwa kipindi cha ‘The Late Show’, mwanadada huyo ambaye ni mzaliwa wa Houston alikozaliwa Beyonce, alisimulia jinsi alikuwa akitazama kundi la muziki kwa jina “Destiny Child” akiwa mdogo na kujiambia kwamba siku moja angependa kufanya muziki kama wanadada hao.

Kulingana naye watu wa Houston wanamenzi sana Beyonce.

Megan alipata nafasi ya kurudia wimbo wake kwa jina “Savage” akimshirikisha Beyonce mwezi wa nne mwaka huu na kibao hicho kilitazamwa zaidi ya mara milioni 58 kwenye Youtube.

Alipoulizwa ni nani kati ya Beyonce na Jay Z ambaye humpa ushauri mzuri, Megan alisema Jay Z humpa ushauri unaolenga kujivinjari naye Beyonce humhimiza kutia bidii na kusonga mbele.

Megan aliyeanza kazi ya muziki mwaka 2016 sasa ana albamu ambayo ameipa jina la “Good News yaani “habari njema” kisa na maana alitaka watu wapate habari njema mwaka huu mgumu wa 2020.

Ameteuliwa kuwania tuzo za Grammy kwenye vitengo vinne, akatajwa kuwa miongoni mwa watu mia moja wenye ushawishi mkubwa na jarida la Times, nalo jarida la GQ likamtawaza rapper wa mwaka.

Mwaka huu una mazuri mengi kwa binti huyu wa miaka 25 lakini pia alikwazika na uzani alioupata wakati wa virusi vya Corona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *