Shule kufunguliwa tena Msumbiji baada ya kufungwa kwa mwaka mmoja

Msumbiji imetangaza kufunguliwa kwa shule kuanzia Jumatatu ijayo baada ya kufungwa kwa mwaka mmoja kutokana na janga la ugonjwa wa Covid-19.

Rais Felipe Nyusi alisema kuwa hatari ya maambukizi ya ugonjwa huo katika shule sasa imepungua.

Alisema kuwa hata hivyo shule zitahitajika kufwata maagizo ya wizara ya afya kuzuia maambukizi kwa kupunguza baadhi ya shughuli za shule.

Baadhi ya shule zitafunguliwa baadaye, huku nyingine zikipunguza kutangamana kwa karibu kwa wanafunzi.

Agizo hilo linahusu viwango vyote vya elimu,japo shule za chekechea hazikutajwa kwenye hotuba hiyo ya rais.

Walimu waliliambia shirika la utangazaji la Uingereza-BBC kuwa wanaunga mkono agizo hilo la rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *