Shujaa yashinda mechi zote tatu Madrid 7’s

Timu ya taifa ya raga ya wanaume 7 kila upande imeshinda mechi zote tatu za siku ya kwanza ,mzunguko wa pili wa mashindnao ya Madrid 7 nchini Uhispania Jumamosi Februari 27.

Shujaa chini ya ukufunzi wa Innocent Simiyu walianza vyema kwa kuwazidia maarifa wenyeji Uhispania alama 19-17,kabla ya kuwanyofoa USA 29-12,na kuinyuka Ureno 26 -12.

Baada ya mechi za leo Shujaa ni ya pili kwa pointi 9 sawa na Argentina inayoongoza huku Marekani ikiwa pointi 7.

Kenya itarejea uwanjani Jumapili saa saba na dakika 20 dhidi ya Chile na kufunga ratiba dhidi Argentina saa tisa na dakika 42 .

Timu ya wanawake Kenya Lionnes imeshind amechi moja na kupoteza moja ikiwagaragaza wenyeji Uhispania alama 22 kwa nunge na kupigwa alama 5-17 na Russia.

Mashindano hayo ya Madrid 7’s ya wiki mbili yatakamilika Jumapili huku timu za Kenya zikitumia kujiandaa kwa michezo ya Olimpiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *