Shujaa yaipakata Uganda na Canada ,huku Lionesses wakipigwa kumbo Dubai 7’s

Timu ya taifa ya  raga ya Kenya  kwa wachezaji  7 kila upande ya wanaume, imeanza vyema mkondo wa pili wa mashindano ya Dubai 7’s baada ya kuinyuka Uganda alama 28-10 katika mechi ya kwanza ya kundi lao Alhamisi .

Katika mchuano wa pili Shujaa wanaotumia mashindnao hayo ya mwaliko kujiandaa kwa michezo ya Olimpiki waliititiga Canada 2 pointi 22-10 .

Hata hivyo timu ya wanawake ya Kenya maarufu kama Lionesses imepoteza mechi  mbili za ufunguzi ikipakatwa alama 22-5 na Canada kabla ya kuchabangwa na Ufaransa pointi 31-5 katika ,mechi ya pili.

Mashindano hayo yatakamilika Ijumaa yakiwa katika wiki ya pili, baada ya mkondo wa kwanza kuandaliwa wiki jana ambapo Shujaa iliibuka ya tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *