Sheila Chelangat ahifadhi taji ya kitaifa mbio za nyika

Sheila Chelengat wa Polisi alistahimili  changamoto nyingi ikiwemo baridi na matope na kuhifadhi taji ya kitaifa ya mbio za kilomita 10 katika mashindano ya kitaifa yaliyoandaliwa Jumamosi katika uwanja wa Ngong Race Course.

Chelengat alikuwa katika kundi la uongozi kutoka mwanzo hadi mwisho  na kuongeza kasi katika mzunguko huku  akikata utepe kwa  dakika 34 sekunde 55 nukta 5 akifuatwa na Daisy Cherotich kutoka Central Rift kwa dakika 35 nukta 09 naye bingwa wa dunia katika mbio za marathon Ruth Chepngetich wa Nairobi akaridhika katika nafasi ya tatu .

Agnes Chebet wa Central Rift,Everlyne Chirchr wa Nyanza kaskazini na Hyvin Kiyeng waliambatana katika nafasi za  4,5 na 6 mtawalia huku wote 6 wakifuzu kushiriki mashindano ya mbio za Nyika Afrika tarehe 7 mwezi ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *