Categories
Habari

Serikali yasuluhisha zogo lililoghubika dawa za kupunguza makali ya Ukimwi

Wakenya wanaoishi na virusi vya HIV na ugonjwa wa ukimwi, sasa wana sababu ya kutabasamu baada ya serikali kusuluhisha zogo ambalo liliacha nchi hii ikikodolewa macho na uhaba wa dawa za kukabiliana na makali ya Ukimwi.

Kwenye taarifa iliyotolewa na waziri wa afya, Mutahi Kagwe, alisema zogo hilo limesuluhishwa na dawa hizo sasa zimeidhinishwa kusambazwa.

Hofu iliongezeka miongoni mwa Wakenya wanaoishi na virusi vya HIV na ugonjwa wa ukimwi kufuatia mzozo kati ya serikali ya Kenya na ile ya Marekani kuhusu kucheleweshwa shehena katika bandari ya Mombasa.

Kagwe kwenye taarifa alisema wizara ya afya imepokea idhini ya kusambaza dawa hizo.

Alisema hali inayojiri kwa sasa haikutarajiwa na serikali ilifahamu tu kuhusu uwezekano wa kuchelewa dawa hizo mwezi Januari, akisema kuchelewa kusambazwa dawa hizo ni hali ya kusikitisha.

Kagwe alisema wizara ya afya imepokea baadhi ya dawa kutoka sehemu nyingine na inasambaza dawa hizo katika taasisi za afya kote nchini ili kuhakikisha wagonjwa wanaendelea kuzipokea.

Shirika la USAID lilikuwa limekataa kuidhinisha usambazaji dawa hizo kwa nchi hii na ya serikali kuitisha ushuru wa shilingi milioni 45.8 kwa michango ya huduma za afya, hatua ambayo ilisababisha shehena hiyo kukwama katika bandari ya Mombasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *