Serikali yafuatilia wanafunzi wote ili hata mmoja asikose kurejea masomoni

Wizara ya Elimu sasa inakusanya orodha ya wanafunzi wote waliokuwa shuleni kote nchini kabla shughuli za masomo kusitishwa kufuatia chamko la ugonjwa wa COVID-19 mnamo mwezi Machi mwaka uliopita.

Kulingana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Belio Kipsang, hatua hiyo itasaidia kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wamerejelea masomo.

Dkt. Kipsang amesema kuwa serikali pia inatafuta taarifa kuhusu wanafunzi wa kike ambao huenda walitungwa mimba wakati shule zilipokuwa zimefungwa.

Taarifa kuhusu shuleni walikokuwa wakisomea wasichana hao, madarasa walimokuwa na hatua walizofika katika uja uzito wao zinakusanywa ili kuhakikisha kwamba wanarejelea masomo pasi na changamoto nyingi.

Katibu huyo ameeleza nia ya serikali ya kuhakikisha kwamba hakuna mwanafunzi anayeachwa nyuma katika ufunguzi wa shule bali wanafunzi wote wanarejelea masomo kwa asilimia 100.

Aidha, Dkt. Kipsanga amesema serikali imetenga takriban shilingi bilioni 30 kwa ajili ya uimarishaji wa miundo msingi katika shule za msingi na za upili za umma kote nchini.

“Shule za msingi za malazi za gharama ya chini zinazopatikana katika maeneo kame zimetengewa shilingi milioni 300,” amesema Dkt. Kipsang.

Kipsanga amesema haya alipozuru Shule ya Msingi ya St. Mary’s, ile ya Sekondari ya Kaplong, Tenwek na Korara katika Kaunti ya Bomet.

Alikuw aameandamana na Kamishna wa kaunti hiyo Susan Waweru na Mkurugenzi wa Elimu wa kaunti hiyo Indiatsi Mabale pamoja na maafisa wakuu wa usalama wa eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *