“Serikali tafadhali mchukulie hatua!” Msizwa

Aliyekuwa mume wa dadake Diamond Platnumz, Esma Platnumz, Msizwa sasa anaiomba serikali ya Muungano wa Tanzania imchukulie hatua.

Haya yanajiri baada ya mke huyo wake wa zamani kukiri kwamba aliavya mimba yake mwisho wa mwaka jana.

Esma alikuwa mubashara kwenye akaunti yake ya Instagram ambapo alikiri kwamba aliavya mimba hiyo kwa sababu hakumpenda Msizwa na hangestahimili mtoto ambaye pia labda hangempenda.

Alikuwa akijibu maswali ya wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii wakati alifichua hayo. Mwisho wa mwaka jana mwanadada huyo alilazwa hospitalini kwa muda na hakuna ambalo lilisemwa kuhusu alichokuwa akiugua.

Baada ya kufahamu hayo msizwa aliisihi serikali imchukulie hatua kwani uavyaji mimba ni hatia nchini Tanzania.

Kulingana naye hicho sio kitu cha kujivunia na kwamba hakumwambia moja kwa moja akipanga kufanya vile lakini alijuzwa na rafiki za Esma.

Wakati Esma alikuwa hospitalini mwaka jana, Msizwa aliweka picha ya mshumaa kwenye Instagram na kuandika “Binadamu hawana huruma” kama ambaye alikuwa anaomboleza jambo ambalo lilisababisha wafuasi wao kwenye mitandao ya kijamii waanze kukisia.

Ndoa ya Msizwa na Esma ilidumu miezi kadhaa na hata Esma akiwa hospitalini mwisho wa mwaka jana, Msizwa alikuwa nchini AfrikaKusini na mke wake mwingine.

Mfanyibiashara huyo anasema kufikia sasa amerudishiwa gari la kifahari aina ya “BMW X6” ambalo alimpa Esma kama zawadi wakati wa arusi yao.

Msizwa pia anaelezea kwamba yeye hakumtaliki Esma na kwamba alijipa talaka mwenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *