Serena Williams azimwa nusu fainali Us Open

Ndoto ya Serena Williams wa Marekani kushinda taji ya 24 ya Grand slam ,yamezimwa baada ya kubanduliwa nje ya  mashidnano ya Us Open na Victoria Azarenka wa Belarus katika nusu fainali mapema leo.

Williams aliye na miaka 38 alianza vyema semi fainali hiyo huku akishinda seti ya kwanza 6-1 ,lakini akapoteza seti zilizofuatia 3- na 3-6 kwa Azarenka ambaye pia aliandikisha historia kumshinda Mmareakni huyo kwa mara ya kwanza katika mechi 10 walizokutana  ikiwemo fainali yam waka 2012 na 2013 .

Katika nusu fainali nyingine Naomi  Osaka kutoka Japan anayeorodheshwa wa 4 ulimwenguni alimbwaga Jennifer Brad wa Marekani seti 2-1  .

Osaka alipoteza seti ya kwanza 7-6, kabla ya kuimarisha mchezo wake na  kushinda 3-6 na 3-6 .

Naomi Osaka baada ya kufuzu fainali-picha hisani ya Cris Oddo

Fainali ya mapema jumapili itakuwa kati ya Azarenka mwenye umri wa miaka 31 na Osaka  atakayecheza fainalib ya  Us Open kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *