Serena kumenyana na Azarenka nusu fainali US Open

Serena  Williams alistahimili wakati mgumu ,kabla ya kumlemea Tsvetana Pironkova kutoka Bulgaria  seti 2-1 na kufuzu kwa nusu fainali ya mashindano ya US Open.

Serena aliye na umri wa miaka 38 alipoteza seti ya kwanza 4-6 ,kabla ya kushinda seti mbili zilizofuatia 6-3 na 6-2 kwenye robo fainali.

Mmarekani huyo  atachuana na bingwa wa zamani wa dunia Victoria Azarenka wa Belarus , katika nusu fainali,ikiwa ni mara ya tatu kwa wawili hao kukutana katika mashindano ya Us Open baada ya Serena kumshinda mwaka 2012 na 2013 katika hatua ya fainali.

Azarenka alifuzu kwa nusu fainali kufuatia ushindi wa seti 2-0 za 6-1 na 6-0  dhidi ya Elise Mertens kutoka Ubelgiji .

nusu fainali ya mapema kesho baina ya Azarenka na Serena itatanguliwa na semi fainali  kati ya  Jennifer Brady wa Marekani dhidi ya Naomi Osaka wa Japan.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *