Seneta Ron Johnson wa chama wa Republican athibitishwa kuwa na Covid-19

Seneta wa chama cha Republican Ron Johnson amethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Covid-19 lakini yaonekana haonyeshi dalili za ugonjwa huo kwa mujibu wa msemaji wake.

Seneta huyo anayeongoza kamati ya usalama wa ndani na masuaa ya serikali katika seneti,  ataendelea kujitenga hadi atakaposhauriwa na daktari kulingana na msemaji wake.

Hawakueleza jinsi alivyoambukizwa ugonjwa huo.

Johnson ni seneta wa tatu wa chama cha Republican kuthibitishwa kuwa na ugonjwa huo katika kipindi cha siku mbili zilizopita, baada ya Thom Tillis na Mike Lee.

Wengine ni aliyekuwa mshirika wa rais Trump Kellyanne Conway, meneja wa kampeni wa Trump Bill Stepien, mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya chama cha Republican-RNC Ronna McDaniel, na washirika wengine watatu wa ikulu ya White House.

Haya yanajiri huku Rais wa nchi hiyo Donald Trump akiendelea kutibiwa covid-19 katika hospitali moja ya kijeshi nchini humo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *