Semenya kuendelea kupinga sheria katili za riadha

Bingwa wa dunia na Olimpiki katika mita 800 Caster Semenya wa Afrika Kusini amesema kuwa bado atapigana dhidi sheria mpya za  kimataifa katika riadha  licha ya kupoteza rufaa juzi katika mahakama ya CAS.

Semenya alikuwa amewasilisha rufaa kwa Cas  kupiga sheria mpya za shirikisho la riadha duniani zilihitaji wanariadha walio na hormone nyingi za kiume yaani Testesterone kama yeye kufanyiwa matibabu ya kunguza viwango vya homoni hizo ili kurusiwa kushiriki mashindano na wanawake.

La sivyo pia wanariadha wenye sampuli hiyo ya ki maumbile wataruhisiwa kushiriki mashindano ya riadha ya wanawake  katika umbali wa kuanzia mita 1500 na zaidi .

Kufuatia uamuzi wa mahakama ya CAS  huko kudumisha sheria hiyo,ina maana kuwa Semenya aliye na miaka 29 hataruhisiwa kutimka mbio za mita 800.

Kulingana na jarida la afrika kusini ,The Citizen .co.za Semenya aliahidi kuendelea kupinga sheria hizo mpya “nitaendelea kupigania haki za wanariadha wa kike ,ndani nan je ya uwanja hadi turuhisiwe kukimbia huru jinsi tulivyozaliwa,”Akasema Semenya

Semenya ambaye ni bingwa mara mbili wa Olimpiki hajaruhusiwa kushiriki mashindanoni tangu Julai mwaka jana alipopoteza rufaa katika mahakama ya CAS.

Hapo jana ,Chama cha riadha Afrika kusini pia ASA pia kimetangaza kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa CAS bila kutoa maelezo Zaidi.

Uamuzi huo umewaathiri wanariadha wenye maumbile ya kiume kama vile Francine Niyonsaba wa Burundi pamoja na wakenya kadhaa ambao wamefungiwa kushiriki mashindano tangu mwaka uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *