Samba Boys wakosa adabu za mgeni na kuwatesa Uruguay

Mabingwa mara tano wa dunia Brazil waliendeleza rekodi yao ya asilimia 100 waliposajili ushindi wa mabao 2-0  dhidi ya Uruguay ugenini mjini Montevideo Uruguay katika mchuano wa kufuzu kwa dimba la kombe la dunia uliosakatwa mapema Jumatano.

Brazil Ukipenda Samba Boys walikamilisha kibarua katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo kupitia kwa mabao 2 ya Arhur na Richarlson  huku mshambulizi wa Uruguay Edinson Cavani akilishwa kadi nyekundu kwa mchezo mbaya wakati Luis Suareza akikosa pambano kutokana na kuugua homa ya Corona.

Brazil wakichuana na Uruguay

Katika matokeo mengine Argentina pia ilipata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya  Peru Nicolas Gonzalez na Lautaro Martinez wakipachika mabao ya ushindi katika kipindi cha kwanza.

Venezuela pia walisajili ushindi wa kwanza kwa kuikung’uta  Chile mabaoa 2-1 wakati Bolivia na Paraguay wakitoka sare ya 2-2 nayo Ecuador ikaichakaza Colombia mabao 6-1.

Brazil wanaongoza msimamo kwa pointi 12 kutokana na mechi 4 wakifuatwa na Argentina kw aalama 10 wakati Ecuador ikiwa na alama 9 wakati Paraguay na Uruguay zikizoa pointi 6 kila moja.

Mechi za raundi ya 5 hatua ya makundi kuchezwa mwezi Machi mwakani.

Mataifa matano bora  kutoka ukanda huo wa Amerika kusini CONMEBOL yatafuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar huku timu ya 6 ikicheza mchujo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *