Safari za treni kati ya Nairobi na Nanyuki kurejelewa hivi karibuni

Jaribio la treni ya kwanza ya abiria kutoka Nairobi hadi Nanyuki limefanyika mwishoni mwa juma hili na kuashiria mwanzo wa kurejelewa kwa safari za treni kwenye eneo la katikati ya nchi.

Ni hatua inayonuiwa kuimarisha uchumi wa eneo hilo watalii wakitarajiwa kusafiri kutumia reli wakifurahia mandhari ya kuvutia.

Walioabiri treni hiyo ya majaribio walielezea furaha yao kwa kurejelewa kwa huduma za reli kutoka Nairobi hadi Nanyuki.

Gavana wa Lakipia  Mureithi Nderitu, alisema sekta ya utalii inatarajiwa kuimarika kutokana na huduma za reli.

Alisema serikali ya kaunti hiyo itajizatiti kuwavutia wawekezaji katika sekta zinazofungamana na reli.

Muriithi alisema sekta za nyama na uchimbaji madini zitaimarika kwani reli hiyo imetoa nafasi ya usafirishaji bidhaa.

Aidha serikali ilisifiwa kwa kufufua usafiri wa reli ambao ni salama na wa bei nafuu.

Halmashauri ya reli humu nchini sasa inatarajiwa kuanzisha safari za kutoka Nairobi kwenda Nanyuki ili kutoa nafasi kwa wakenya kufurahia usafiri kwa njia ya reli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *