Safari ya kwenda Qatar kutoka Ulaya kuanza Machi 2021

Mataiafa ya Ulaya 55 yataanza mechi za makundi kufuzu kwa dimba la kombe la dunia nchini Qatar baina ya Machi na Novmber mwaka ujao.

Kwa mjibu wa droo iliyoandaliwa Jumatatu usiku mjini Zurich Uswizi mataifa hayo 55 yametengwa katika makundi 10 huku timu itakayoongoza kila kundi baada ya mechi za makundi zikifuzu kwenda kombe la dunia .

Mataifa 10 bora katika nafasi za pili kutoka kila kundi na timu 2 bora kutoka mashindano ya UEFA Nations League yatajumuishwa pamoja kwenye droo kila timu ikicheza mchujo  na wapinzake wake wawili huku timu 3 bora zitakazoshinda pia zikijikatia tiketi kupiga kombe la dunia nchini Qatar kati ya Novemba na Disemba mwaka 2022.

Michuano ya mchujo itapigwa Machi mwaka 2022.

Bara ulaya litawakilishwa na mataifa 13  kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2022,wakati Afrika ikitengewa nafasi 5,Asia nafasi 4,Marekani Kusini nafasi 4 ,

eneo la Conacaf nafasi 3,Oceania nafasi 1 au 0,waandalizi Qatar huku nafasi nyingine  zikijazwa kupitia michujo baina ya mabara.

Tayari bara Amerika Kusini limecheza mechi nne   za makundi za kufuzu kwa kombe la dunia huku bara Afrika ikipanga kuanza michuano yake mwezi Juni mwaka ujao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *