S2kizzy kufanya kazi na Amber Rose mwakani

Mtayarishaji muziki au ukipenda “producer” maarufu nchini Tanzania S2Kizzy Zombie ni mwingi wa furaha baada ya kuwasiliana na mwanamitindo na muigizaji wa Marekani ambaye pia anapenda muziki Bi. Amber Rose.

S2Kizzy anasema hakuamini alipopokea ujumbe wa moja kwa moja kwenye akaunti yake ya Instagram kutoka kwa nyota huyo wa Marekani.

Anasema mwanadada huyo alisifia kazi yake ya muziki na kwamba angependa kufanya kazi naye. Zombie anasema alikuwa kwenye safari ya kurejea kutoka Mbeya kwa ziara ya “tumewasha na Tigo” wakati ujumbe huo uliingia.

Hakujua jinsi ya kuujibu na akalazimika kuomba ushauri kwa waliokuwa naye safarini ambao inaaminika ni watu wa familia ya Wasafi Media ambao walimwelekeza kwenye mawasiliano hayo.

Akizungumza wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha “The Switch” cha Wasafi Fm, S2kizzy alifichua kwamba tayari wamekubaliana na Amber Rose kufanya kazi ya muziki mwaka ujao wa 2021.

Amber Rose hajakuwa akizingatia sana kazi ya muziki lakini ana vibao kadhaa. Mwezi Januari mwaka 2012 alizindua kibao cha kwanza kwa jina “Fame” akimshirikisha Wiz Khalifa, mwezi wa pili mwaka huo wa 2012 akaangusha kibao kingine kwa jina “loaded” na baadaye akashirikiana na aliyekuwa mume wake Wiz Khalifa kwenye kibao cha “Rise Up”.

Tangu wakati huo mwanadada huyo ambaye sasa ni mama wa watoto wawili hajajihusisha na muziki na inaonekana kwamba ataurejelea mwakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *