Categories
Michezo

Rwanda na Tanzania kuandaa mechi za Cecafa kufuzu kombe la Afcon kwa chipukizi

Shirikisho la Cecafa limetangaza kuandaliwa kwa mechi za kanda hii kufuzu kwa kombe la Afcon kwa vijana chipikuzi mwezi Novemba na Disemba mwaka huu.

Kulingana na maafikiano ya baraza kuu la Cecafa mjini Arusha Oktoba 10 ,Cecafa itaandaa mechi

za kufuzu kwa kombe la Afcon kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 20   baina ya Novemba 22 na Desemba 6 nchini Tanzania .

 

 

Mataifa yalitoa ithibati  kushiriki ni pamoja na Somalia,Burundi,Tanzania

Uganda,South Sudan,Sudan,Eritrea,Djibouti,Ethiopia na Kenya.

Timu hizo  10 zitatengwa katika makundi mawili ya 5 kila moja kulingana na droo itakayoandaliwa kwa njia ya ki elektroniki huku mataifa mawili bora kutoka kila kundi yakifuzu kwa nusu fainali .

Mashindano  ya kombe la Afcon kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 yataandaliwa nchini Mauritania baina ya  Februari na Machi mwaka ujao.

Kwa mjibu wa Cecafa pia Rwanda imeteuliwa kuwa mwenyeji wa mashindnao ya kufuzu kwa kombe la Afcon kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17 kati ya Desemba 13 na 28 .

 

 

Nchini 10 zitakazoshiriki ni Rwanda,Burundi,Ethiopia,Sudan,South Sudan,Kenya,Uganda na Tanzania ,Eritrea na Djibouti.

Timu hizo pia zitatengwa katika makundi mawili huku timu mbili bora kutoka kila kundi zikifuzu kwa nusu fainali.

Mashindano ya Afcon U 17 yataandaliwa nchini Moroko Julai mwaka ujao .

Timu mbili kutoka ukanda wa Cecafa zitafuzu kwa kila mashindano hayo ya mwaka ujao.

Cecafa imewataka waandalizi wa mashindano hayo ya mwezi ujao na Desemba kuzingatia masharti ya afya kuhusu ugonjwa wa Covid 19.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *