Rs Berkane watinga fainali kombe la shirikisho Caf

Kapteini Mohammed Aziz alifunga penati mbili katika kila kipindi na kuwasaidia Rs Berkane kutoka Moroko kutinga fainali ya kombe la shirikisho la soka barani afrika Caf Jumatatu usiku kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenzano Hassania Agadir pia ya Moroko  mjini Rabat .

Berkane walipoteza kwenye fainali ya mwaka jana dhidi ya Zamalek , watachuana na mshindi wa nusu fainali ya pili Jumanne usiku kati ya  Pyramids kutoka Misri dhidi ya  Horoya AC ya Guinea kwenye fainali ya jumapili.

Agadir walikuwa wakiwinda kucheza fainali ya kombe hilo kwa mara ya kwanza lakini azma yao ikakatizwa na wenzao Berkane.

Nusu fainali ya pili kupeperushwa mbashara na runinga ya Kbc Channel 1 kuanzia saa nne usiku wa Jumanne.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *