Rs Berkane watawazwa mabingwa wa kombe la Caf Confed

Mohssine Iajour alipachika bao la pekee la mchezo na kuisaidia  RS Berkane ya Moroko kuwabwaga Pyramids ya Misri bao 1 kwa bila na kunyakua kombe la shirikisho la soka afrika Caf Jumapili usiku.

Mchuano huo uliosakatwa katika uwanja wa June 30 jijini Cairo  ulilkuw na msisimko wa aina yake  huku Iajour akipachika bao hilo katika dakika ya 15.

Berkane walipata fursa ya kulipiza kisasi baada  ya kupoteza kwenye fainali ya kombe hilo mwaka uliopita  dhidi ya Zamalek.

Hata hivyo Berkane walilazimika kumaliza wachezaji 10 uwanjani sawia na kwenye fainali ya mwaka jana baada ya baada ya Bakre El Helali kupigwa kadi nyekundu kwa mchezo mbovu.

Pyramids walikuwa wakicheza fainali hiyo kwa mara ya kwanza wakipoteza mechi  2 pekee kati ya 15 walizocheza na kujivunia kutopoteza mechi yoyote ugenini msimu huu.

Berkane ni timu  ya tano kutoka Moroko kushinda kombe hilo wakisawazisha rekodi ya Tunisia ambao pia wametwaa taji hiyo mara tano na kupokea dola milioni 1 nukta 25 za Kimarekani  .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *