Riadha Kenya yaadhimisha miaka 70 huku maslahi ya wanariadha yakitakiwa kupewa kipa umbele

Mabingwa wa dunia Hellen Obiri na Timothy Cheruiyot na mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za nusu marathon Kibiwott Kandie ni miongoni mwa magwiji wa sasa waliojitokeza kuhudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 70 tangu kubuniwa kwa chama cha riadha Kenya mwaka 1950.

Obiri ambaye ni bingwa wa dunia katika mita 5000 ameirai serikali kuwaweka wanariadha wastaafu katika mpango maalum ambapo watakuwa wakilipwa kiwango fulani cha pesa za kujikimu  na kuwapa bima ya matibabu .

“Mimi naiomba serikali tunapoadhimisha miaka 70 itafute njia ya kuwaweka wanariadha wastaafu  kwa malipo kidogo ya kila mwezi na kuwawekea bima ya matibabu ili kujikimu kama njia ya kuwatambua na kuwaenzi”akasema Obiri

Obiri  ambaye ni wa  kikosi cha KDF wakati huo huo pia amesema amaerejea mazoezini huku akishiriki mashindano ya mwishoni mwa juma hili ya mbio za Nyika huko Nandi kama njia moja ya kujiweka sawa kwa michezo ya Olimpiki mwaka ujao.

“Kwa sasa nimerejea mazoezini na nilishiriki mashindano ya mbio za nyika huko Machakos na nitakuwa Nandi wikendi hii kushiriki mkondo wa pili wa mbio za nyika nchini “akaongeza Obiri

Kwa upande wake  Kibiwott Kandie  ambaye ameshinda mbio za nusu marathon za Valencia na kuandikisha rekodi ya dunia  amesema  anajivunia sherehe hizi na kusema angali mapumzikoni kabla ya kurejea uwanjani mwaka ujao akilenga dhahabu ya Olimpiki  mita 10000.

“Najivunia rekodi ya dunia ya nusu marathon huku AK ikiadhimisha miaka 70 ,kwa sasa niko mapumzikoni kabla ya kurejea mashindanoni huku nikilenga kushiriki mita 10000 katika michezo ya Olimpiki mwaka ujao”akasema Kandie

Bingwa Olimpiki mwaka 1972 Charles Asati

Baadhi ya viongozi waliohudhuria hafla ya Jumanne uwanjani Nyayo ni Gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago aliyeahidi kuwa serikali yake inajenga uwanja mpya wa nyanda za juu utakaowasaidia wanariadha kufanya mazoezi na kuwa na uwezo wa kuandaa mashindano ya kimataifa.

“Nimekuja hapa kusherehekea Ak @70 kwa sasa najenga uwanja wa 64 mjini Eldoret na pia kujenga uwanja wa kisasa wa nyanda za juu ili kuwakuza wanariadha zaidi”akasema Gavana Mandago

Gavana wa Nyeri ambaye ni mwanariadha mstaafu na afisa wa zamani wa chama cha riadha Mutahi Kahiga kwa upande wake alisema alikuja kusherehekea jamii ya riadha huku akitangaza kuwa kaunti yake inakaribia kukamilisha ujenzi wa uwanja wa Ruring’u  kwa ushirikiano na serikali ya kitaifa.

“Imebidi nihudhurie sherehe ya leo hapa kwnai nilikuwa mwanariadha zamani kabla ya kuwa afisa wa chama cha riadha Kenya na kile nimefanya katika kaunti yangu ni kuharakisha ujenzi wa uwanja wa Ruring’u”akasema  Gvana Kahiga.

Waziri wa michezo Dr Amina Mohammed ,seneta wa Kisii  Prof Sam Ongeri ambaye alikuwa hafla hiyo mwenyekiti wa zamani wa chama cha riadha Kenya

walihudhuria .

Wanariadha wakongwe  waliotuzwa ni pamoja na bingwa wa Olimpiki mwaka  1978 katika mita 400 kupokezana kijiti  Charles Asati,mshikillizi wa zamani wa rekodi ya kitaifa Rose Tata Muya ,bingwa wa dunia mwaka 2005 katika mita 5000 Benjamin Limo na bingwa mara tano wa dunia katika mbio za nyika Paul Tergat miongoni mwa wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *