Rekodi ya dunia yamkwepa Faith Kipyegon kwa mara ya 3

Matumaini ya bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 1500, Faith Chepngetich Kipyegon kuvunja rekodi ya dunia katika mita 1000 yaligonga mwamba kwa mara ya tatu mwaka huu katika mashindano yaliyoandaliwa Jumamosi Usiku mjini Hengelo Uholanzi.

Kipyegon aliye   na umri  wa miaka 26 aliibuka mshindi wa  mbio lakini akakimbia kwa muda wa dakika 2 sekunde 32 nukta 82 nje ya rekodi ya dunia iliyoandikishwa na Mrusi Svetlana Masterkova miaka 16 iliyopita ya dakika 2 sekunde  28 nukta 98.

Ilikuwa mara ya tatu kwa bingwa huyo  wa dunia wa mwaka 2017 kujaribu kuvunja rekodi ya mita 1,000 baada ya kutimka kwa dakika 2 sekunde 29 nukta 15 katika mkondo wa Moanco Diamond league Agosti 14 mwaka huu , akikosa nukta 17 pekee avunje rekodi hiyo.

Kipyegon aliwekewa kasi na mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mita 3000 kuruka viunzi na maji Beatrice Chepkoech.

Baadae alitumia dakika 2 sekunde 29 nukta 92 kukamilisha shindano la mita 1000 katika mkondo wa Brussels Diamond league Septemba 4 mwaka huu.

Katika mbio za Jumamosi ,Winnie Nanyondo wa Uganda aliibuka wa pili nyuma ya kipyegon kwa dakika 2 sekunde 40 nukta 50 huku  Eunice Suma akitwaa nafasi ya tatu akifuatiwa na bingwa wa Olimpiki katika mita 3,000 kuruka viunzi na kidimbwi cha maji Beatrice Chepkoech .

Pia harakati za Yomif Kejelcha wa Ethiopia  na Sifan Hassan wa Uholanzi  kuvunja rekodi za mita  5,000 kwa wanaume na mita 10,000 kwa wanawake mtawalia yaliambaulia pakavu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *