Raymond Oruo ateuliwa kaimu Ceo Gor Mahia

Raymond Oruo ameteuliwa kuwa kaimu Ceo katika kilabu ya Gor Mahia ambapo pia atakuwa mshauri mkuu na kusimamia masuala ya mauzo.

Oruo anaingia Gor akiwa na Tajriba pana baada ya kuhudumu katika wadhfa huo katika benki ya KCB akisimamia shughuli nyingi za michezo ikiwemo klabu ya soka ya Kcb  na atafanya kazi chini ya katibu mkuu wa timu Sam Ochola.

Gor hawajakuwa na afisa mkuu mtendaji tangu kujiuzulu kwa Lordvick Aduda anayewania Urais wa Fkf katika uchaguzi wa mwezi ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *