Ratiba ya ligi kuu ya FKF kubainika Jumatano

Usimamizi wa ligi kuu  ya Fkf umetangaza kutangaza ratiba ya msimu mpya Jumatano hii Oktoba 14 huku msimu mpya wa mwaka 2020/2021  ukitazamiwa kuanza Novemba 20 mwaka huu.

Kulingana na taarifa kwa vyombo habari ,baraza kuu la ligi ya Fkf limesema kuwa litakutana Jumatano hii kuunda ratiba ya mechi huku wakitoa mapendekezo kwa wizara ya michezo kuwa itakuwa bora kwa msimu mpya kuanza Tarehe 20 mwezi ujao,la sivyo itakuwa vigumu kwa ligi hiyo kuanza.

Baraza kuu la Fkf Premier league limeongeza kuwa kufuatia kuandaliwa kwa mchuano wa kirafiki katia ya Kenya na Zambia  kwa njia ya kufana wiki jana kwa kuzingatia masharti ya Covid 19 kutoka kwa wizara ya afya ,wizara ya michezo inapaswa kuruhusu kuanza kwa msimu  wa ligi na soka humu nchini.

Vilabu vitapewa ratiba hiyo ili kuanza matayarisho kwa msimu mpya kwa wakati ufaao.

Ligi hiyo itafadhiliwa na kampuni ya Betking kutoka Nigeria kwa mkataba wa miaka mitano kwa kima cha shilingi bilioni 1 nukta 2 huku kila timu kati ya vilabu vyote 18 katika ligi vikitarajiwa kunufaika na ruzuku ya shilingi milioni 8 katika kila msimu.

Pia kwa mara ya kwanza baada ya  Subira ya muda mrefu ligi hiyo itakuwa na mfadhili wa Runinga ambapo mechi hizo zitapeperushwa kenyekenye kupitia runinga ya Star Times kutoka China.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *