Raja Casablanca yatwaa taji ya ligi kuu Moroko
Kilabu ya Raja Casablanca ilitwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Moroko maarufu kama Botola ,Jumapili iliyopita wakati wa mechi za kufunga msimu.
Raja walivishwa ubingwa kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya FAR Rabat .
Taji hiyo ilikuwa ikiwaniwa na timu tatu za Raja Casablanca , watani wa jadi Wydad Casablanca na RS Berkane kufikia mechi za kufunga msimu Jumapili iliyopita .
Raja walihitaji tu ushindi katika pambano lao ili kuvishwa taji nao Wydad na Berkane wapoteze .
Ilikuwa mara ya nne kwa Raja kunyakua ubingwa wa ligi hiyo ya Botola tangu mwaka 2012/2013 na la 12 kwa jumla .
Hata hivyo timu za Olympique Khourigba na Raja Benni Melal ziliteremshwa ngazi kutoka ligi kuu Khouriba wakipoteza 1-2 ugenini kwa Moghreb Tetouan huku Benni Melal wakitoka sare ya 1-1 na Renaissance Zemamra.