Rais wa zamani wa FKL Mohammed Hatimy afariki

Aliyekuwa Rais wa shirikisho la kandanda nchini Football Kenya Limited  Mohammed Hatimy  ameaga dunia mapema leo katika Hospitali ya Mombasa kutoka na ugonjwa wa Covid 19 .

Hatimy alikuwa amelazwa katika Hospitali hiyo katika kitengo cha wagonjwa mahututi kwa wiki moja iliyopita na alihudumu kama Rais wa FKL baina ya mwaka 2005 hadi  2011.

Rais wa FKF Nick Mwendwa ameongoza jamii ya soka nchini kuomboleza kifo cha Hatimy akimtaja kuwa kiongozi aliyejituma na kujitolea kwa kazi yake .

Rais mstaafu wa FKF Sam Nyamweya pia amemwomboleza marehemu waliyefanya kazi kwa pamoja kwa muda mrefu kabla ya kumkabidhi uongozi mwaka 2011 aliposhinda uchaguzi.

Baada ya kuondoka katika soka ,Hatimy pia amehudumu  kama mwakilishi wa kaunti mteule  katika bunge la Mombasa na alikuwa mwenyekiti wa kamati ya fedha ya chama cha ODM kaunti ya Mombasa.

 

One thought on “Rais wa zamani wa FKL Mohammed Hatimy afariki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *