Rais wa zamani wa Burundi Pierre Buyoya amefariki

Aliyekuwa Rais wa Burundi Pierre Buyoya ameaga dunia akiwa na umri wa miaka-71. Taarifa hizo za tanzia zimethibitiswa na binamuye Rais huyo wa awali sawa na duru za Kibalozi zinazoarifu kuwa  Buyoya aliaga dunuia jana jijini Paris Ufaransa, kutokana na ugonjwa wa Korona.

Buyoya aliyekuwa Meja mstaafu alihudumu kwa mihula miwili ya jumla ya miaka-13 baada ya kuwapindua watangulizi wake.

Mwezi Oktoba mwaka huu, Buyoya alihukumiwa kifungo cha maisha bila yeye kuwapo mahakamani, nchini Burundi.

Alishutumiwa kwa mauaji ya Rais wa kwanza kuchaguliwa Kidemokrasia nchini Burundi, Elchior Ndadaye mwaka 1993 tukio lililosababisha vifo vya watu elf-300 lakini aliyakanusha madai hayo.

Baadaye Buyoya alichukua hatamu za uongozi wa taifa hilo hadi mwaka 2003 ambapo alijiondoa uongozini kufuatia mkata wa mwaka 2000 wa Arusha uliokusudia kusitisha mzozo.

Baada ya kustaafu,Buyoya alihudumu kama mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika nchini Mali na baadae eneo la Sahel kati ya mwaka 2012 na Novemba 2020.

Mwezi uliopita alijiuzulu kuwa mjumbe wa Jumuia ya Afrika katika eneo la Sahel akisema alinuiwa kuzingatia zaidi harakati za kulisafisha jina lake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *