Rais wa Tanzania Suluhu Hassan awasili Kenya kwa ziara ya siku mbili

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko humu nchini kwa ziara rasmi ya siku mbili.

Rais Suluhu alilakiwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta na waziri wa mashauri ya nchi za kigeni, Raychelle Omamo.

Baadaye Rais Suluhu alipokelewa kwenye ikulu ya rais jijini Nairobi kwa taadhima kuu ikiwemo mizinga 21.

Taarifa ya wizara ya mashauri ya nchi za kigeni imesema viongozi hao watashauriana kuhusu jinsi ya kuimarisha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili.

Taarifa hiyo inasema Kenya imewekeza pakubwa nchini Tanzania huku bidhaa zake zinazouzwa nchini humo zikiongezeka katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Rais Hassan pia atakutana na wadau wa sekta ya biashara kutoka mataifa hayo mawili kujadili fursa za uwekezaji na biashara.

Aidha atahutubua kikao cha pamoja cha bunge la taifa na lile la Seneti siku ya Jumatano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *