Rais wa FIFA Infantino atua Cameroon kufungua CHAN

Rais wa FIFA Gianni Infantino  amewasili mjini Younde  Cameroon mapema ijumaa tayari kufungua rasmi makala ya 6 ya fainali za kombe la CHAN Jumamosi jioni.

Kaimu Rais wa CAF  Constant Omari  na nyota wa soka Afrika Samuel Etoo walimpokea Infantino punde alipowasili .

Infantino anatarajiwa kuongoza  kikao na baraza kuu la CAF Ijumaa ambapo atamtawaza kinara wa zamani wa CAF  Issa Hayatou  .

Mechi ya Ufunguzi ya CHAN itapigwa Jumamosi saa moja usiku wenyeji Indomitable Lions wakivaana na Zimbabwe katika uwanja wa  Ahmadou Ahidjo .

Mechi 32 za kipute hicho zitachezwa katika viwanja vinne katika miji mitatu ya Yaounde,Limbe na Doula.

Mataifa 16 yanayowashirikisha wachezaji wanaocheza katika ligi za nyumbani pekee watashiriki mashindano hayo ya wiki tatu huku fainali yake ikipigwa Februari 7.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *