Rais wa Chad Idriss Deby ameaga dunia

Rais  Idriss Deby wa Chad ameaga dunia alipokuwa akitembelea wanajeshi walio katika mstari wa mbele wanaopigana na waasi kaskazini mwa nchi hiyo.

Hayo yamesemwa Jumanne na msemaji wa jeshi la nchi hiyo siku moja tu baada ya Deby kushinda hatamu ya sita ya uongozi.

Kundi la kampeni za Deby lilisema siku ya Jumatatu kuwa Rais huyo alikuwa akienda kutembelea wanajeshi  wanaokabiliana na magaidi.

Waasi walishambulia kituo kimoja cha mpakani siku ya uchaguzi na kuingia umbali wa kilomita kadhaa upande wa kusini.

Deby, mwenye umri wa miaka 68, alitwaa mamlaka kupitia maasi ya mwaka  1990 na ni mmoja wa viongozi waliotawala kwa kwa muda mrefu zaidi barani Afrika.

Rais huyo aliahirisha kutoa hotuba yake ya ushindi kwa wafuasi siku ya Jumatatu na badala yake akaelekea kuwatembelea wanajeshi walio katika mstari wa mbele kukabiliana na waasi, kulingana na meneja wake wa kampein ya Deby.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *