Rais wa CAF Ahmad Ahmad alishwa marufuku ya miaka mitano kwa Ufisadi

Kamati  ya maadili ya Shirikisho la Soka ulimwenguni (FIFA) imemfungia miaka mitano Rais wa CAF Ahmad Ahmad, kutojihusisha na masuala ya soka kwa tuhuma za matumizi mabaya ya afisi na   matumizi mabaya ya fedha.

Maamuzi ya kamati hiyo yanajiri  wakati Rais huyo ametangaza  nia ya kugombea muhula wa pili kuongoza  CAF kwenye uchaguzi utakaofanyika mwezi Machi mwaka ujao.

kulingana na uamuzi wa Fifa  Ahmad amepatikana na hatia ya kuchukua zawadi na matumizi mabaya ya fedha akiwa afisini baina ya mwaka 2017 na 2019 ikiwemo safari yake kwenda Hijji huko Mecca akitumia pesa za shirikisho  na kujihusisha na  kampuni ya vifaa vya  michezo ya Tactical Steel.

Fifa inatazamiwa kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu kesi ya Ahmad ndani ya siku 60 zijazo ambapo huenda akapigwa marufuku kuwania muhula wa pili afisini.

Uamuzi wa Jumatatu unajiri  mwaka mmoja  na miezi mitano tangu kinara huyo wa Caf akamatwe na maafisa wa ujasusi wa Ufaransa .

Wakati uo huo Fifa imeongeza muda wa Constant Omari kuendelea kuhudumu kama  kaimu Rais wa Caf baada ya Ahmad ambaye pia ni makamu Rais wa FIFA kupatikana na hatia ufisadi na kupigwa marufuku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *