Rais wa Barcelona na bodi yote wajiuzulu

Rais wa kilabu ya  Barcelona Josep Maria Bartomeu ametangaza kujiuzulu siku ya Jumanne , kuepuka fedheha ya kuondolewa afisini kupitia kura ya kukosa imani naye.

Bartmeu amejiuzulu Jumanne pamoja na wanabodi wote  kumanaanisha kuwa uchaguzi utaandaliwa katika kipindi cha siku 90  kumteua Rais mpya wa timu hiyo ya Katalunya.

Kupitia kwa hotuba yake ya  runinga  Bartomeu amesema kuwa ni uamuzi alioafikia baada ya  kutafakari kwa muda.

Zaidi ya wanachama 20,000 walikua wamekusanya sahihi ya kutaka kumng’atua mamlakani Rais huyo kupitia  kwa kura ya kutokuwa na imani   ambayo sasa haina umuhimu wowote

Bartomeu akitoa hotuba ya kujiuzulu

Victor Font, Joan Laporta na  Jordi Roche  ndio wagombezi wa kiti hicho kumrithi Bartomeu   .

Bartomeu aliye na umri wa miaka , 57, alishika hatamu za kuiongaza Kilabu hiyo kutoka  Sandro Rosell mwaka   2014 ,baada ya kuhudumu kama makamu wa rais wa Rosell .

Upo uwezekano meneja wa Mancity  Pep Guardiolakurejea  Barca kufuatia kujiuzulu kwa Bartomeu  .

Bartomeu alichaguliwa kuhudumu kwa muhula  wa pili mwaka 2015 kwa kipindi cha miaka 6, lakini umaarufu wake ulianza kudorora ndani na nje ya uwanja  huku timu hiyo ikirekodi hasara  ya  euro milioni 97  msimu wa mwaka 2007 an 2008 ilipokosa kunyakua taji yoyote.

Kumekuwa na mzozo kuhusu  wa usimamizi katika timu hiyo uliochangia mshambulizi Lionell Messi kutaka kuigura  mwanzoni mwa msimu huu , kuongezea kwa hali ambapo  wanabodi 6  walikuwa   wamejiuzulu  wakilalama usimamzi duni wa Bartomeu mwezi April mwaka huu .

Muda wa kuhudumu kwa Bartomeu uilikuwa ukamilike mwaka ujao.

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *