Rais Sooronbay Jeenbekov wa Kyrgyzstan ajizulu

Rais Sooronbay Jeenbekov wa Kyrgyzstan alijizulu leo akisema anataka kukomesha mzozo uliotokana na matokeo ya uchaguzi wa ubunge yaliyozua ubishi mapema mwezi huu. 

Maandamano yalizuka baada ya vyama vinavyomuunga mkono Jeenbekov kushinda kwenye uchaguzi huo wa tarehe 4 mwezi huu huku wapinzani wakipinga matokeo hayo wakidai kwamba kura zilinunuliwa.

Matokeo hayo yalifutiliwa mbali baadaye lakini hilo halikusitisha taharuki hiyo.

Kwenye taarifa iliyotolewa na afisi yake, Jeenbekov alisema kuwa hataki kunakiliwa katika historia ya nchi hiyo kuwa rais aliyeruhusu umwagikaji damu na kupigwa risasi kwa raia wake.

Zaidi ya watu 1,200 walijeruhiwa na mmoja kuuawa wakati wa makabiliano baada ya uchaguzi huo baina ya waandamanaji na maafisa wa polisi.

Hatua hiyo imejiri huku wafuasi wa waziri mkuu  Sadyr Japarov, aliyekuwa akihudumu kifungo gerezani kwa utekaji nyara juma lililopita walikusanyika tena leo kushinikiza kwamba Jeenbekov ajiuzulu mara moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *