Rais Kenyatta kuongoza taifa kuadhimisha siku kuu ya Jamuhuri

Huku taifa la  Kenya linapoadhimisha miaka 57 tangu lilipotangazwa kuwa Jamhuri,Rais Uhuru Kenyatta atawaongoza wakenya kuadhimisha siku kuu hii muhimu katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo Jijini Nairobi.

Hotuba ya Rais inatarajiwa kugusia maswala muhimu yanayoathiri taifa hili kwa sasa, yakiwemo msambao wa virusi vya Covid-19,mgomo wa wahudumu wa afya pamoja na mpango wa maridhiano wa BBI.

Hata hivyo Sherehe hizi za mwaka huu zitakuwa za aina yake kwa sababu hakutafanyika nyinginezo sambamba na hizo katika sehemu zingine za nchi wala kusomwa kwa hotuba ya rais.

Hatua hiyo nikutokana na tahadhari ya kutii maagizo ya kupiga marufuku mikusanyiko ya watu ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Covid-19.

Tahadhari ya kuzuia maambukizi ya Corona, yamesababisha wageni elfu-5 pekee kualikwa kuhudhuria sherehe hizo katika uwanja wa taifa wa nyayo ikizingatiwa kuwa uwanja huo unatoshea watu elfu 30.

Kamishna wa kaunti ya Nairobi James Kianda amewaomba wakenya kufwatilia sherehe hizo kupitia runinga.

Sherehe za kuadhimisha siku kuu ya Jamuhuri mwaka mwaka huu zimejiri wakati taifa hii linapojizatiti kujikwamua kutoka kwa janga la Covid-19.

Vile vile shehere hizo zinajiri huku wahudumu wa afya wakigoma kwa madai ya kutelekezwa na serikali za kaunti na ile ya kitaifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *