Rais Kenyatta azindua Ujenzi wa Ulinzi Sports Complex

Rais Uhuru Kenyatta mapema Jumatano ameweka  jiwe la msingi ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo  wa Ulinzi Sports Complex wa kikosi cha Ulinzi nchini KDF  huko Lang’ata Baracks.

Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kumudu watu wapatao 10,000 na utaandaa shughuli nyingi za michezo za Kdf pamoja na  halfa nyingine za Jeshi.

Kikosi cha Ulinzi hushiriki michezo mingi ikiwemo timu ya Ulinzi Stars inayoshiriki ligi kuu ya Kenya,riadha,Voliboli,uvutaji jugwe,masumbwi,uogeleaji na kadhalika.

Rais Kenyatta alionyeshwa ramani ya uwanja huo kabla ya kuweka jiwe la msingi ambapo kampuni ya China Wu Yi itatekeleza ujenzi huo.

Rais Kenyatta ambaye ni Amiri Jeshi mkuu alilakiwa na waziri wa Ulinzi Dkt Monica Juma na kikosi chote cha  KDF kikiongozwa na mkuu wa mwajeshi  Robert Kariuki Kibochi  kwenye hafla hiyo fupi.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *