Rais Kenyatta awapongeza watawa wa Loreto

Rais Uhuru Kenyatta ameipongeza jamii ya watawa wa Loreto kutokana na mwongo mmoja wa huduma zao kwa binadamu, na mchango mkubwa kwa ustawi wa taifa hili.

Rais alisema kwamba kupitia kwa mpango wao wa Kikristo na uwekezaji katika masuala ya elimu, kijamii, na matendo mengine ya kujitolea, watawa wa jamii ya Loreto wamebadili maisha ya watu wengi na kuifanya nchi hii kuwa bora zaidi.

Kiongozi wa taifa ambaye alikuwa akiongea leo katika kituo cha Loreto Mary kilichoko eneo la Karen, kaunti ya Nairobi, alitoa mfano wa mshindi wa tuzo la Nobel na mtetezi wa kimazingira  Marehemu  Profesa Wangari Maathai, Msomi Eddah Gachukia, Lady Justice Joyce Oluoch, Lady Justice Njoki Ndung’u, mwana-habari Julie Gichuru, na mtaalamu wa ushauri Tina Njonjo kuwa baadhi ya wanafunzi wa zamani wa shule za Loreto.

Rais Kenyatta, ambaye binafsi alisomea katika shule ya Loreto Convent, Valley Road aligusia pia miaka yake miwili kama mwanafunzi wa shule hiyo ya msingi ya mseto wakati huo, akisema shule hiyo ilimpa maadili ya mtu anayejali sana bidii na heshima kwa wengine.

Kama sehemu ya sherehe za kuadhimisha miaka 100, Rais alitangaza uamuzi wa serikali kuchangia ujenzi wa shule nyingine ya Loreto katika kaunti ya Kilifi ambayo itahudumia wasichana 500.

Rais aliwataka wanafunzi wa zamani wa shule za Loreto kuanzisha hazina maalum na pia mpango wa misaada ya masomo ili kuwawezesha wale wasiobahatika katika jamii kupata mafunzo kwenye shule za Loreto na akatoa mchango wake  binafsi wa shilingi  million 10 kwa ajili ya mpango huo.

Rais Kenyatta alikuwa akiongea leo wakati alipo-ungana na waumini wa kanisa katoliki kwa ibada maalum ya kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzisha kwa jamii ya watawa wa Loreto katika eneo la Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *