Rais Kenyatta atoa wito wa juhudi za pamoja kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga

Kenya imekariri kujitolea kwake kutekeleza miradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga.

Akiongea wakati wa mkutano wa njia ya video ulioandaliwa Jumatatu, Rais Uhuru Kenyatta alitoa wito wa juhudi za pamoja za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga sawia na juhudi zilizowekwa za kukabiliana na janga la COVID-19.

Rais Kenyatta alisisitiza kwamba kupitia ushirikiano huo, ulimwengu utaweza kukabiliana na vitisho vinavyosababishwa na mabadiliko ya hali ya anga.

Rais Kenyatta alitaja kilimo kama ajenda kuu ya mabadiliko ya hali ya anga barani Afrika akisema asilimia kubwa ya watu wa bara hili hutegemea sekta hiyo kujikimu.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson na wenzake Narendra Modi na Evelyn Wever-Croes wa India na Aruba mtawalia pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres na mtangulizi wake Ban Ki-Moon. Mkutano huo uliandaliwa na waziri mkuu wa Uhalonzi Mark Rutte.

Kwa mujibu wa Rais, wakulima kutoka bara Afrika wanapaswa kupewa habari muhimu na usaidizi wa kifedha ili kuwawezesha kukumbatia mbinu bora za kilimo na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *