Rais Kenyatta aratibiwa kuzungumza katika kikao cha 75 cha Umoja wa Mataifa

Rais Uhuru Kenyatta ameratibiwa kuzungumza Jumatatu jioni kwenye kikao cha 75 cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Mkutano huo utaandaliwa mtandaoni kama njia mojawapo ya tahadhari za kuzuia kuenea kwa virusi vya Korona.

Viongozi wa mataifa wanatarajiwa kuhutubu kupitia kwenye video jijini  New York, Marekani.

Kwenye mkutano huo wa ngazi za juu kwa jina  ‘The Future We Want, the UN We Need’, unaashiria  kuimarishwa kwa ushirikiano wa kimataifa  huku mjadala mkuu ukitarajiwa kufanywa siku ya Jumanne.

Miongoni mwa ajenda nyinginezo ni pamoja na kubuniwa kwa njia mbadala ya kukabiliana na changamoto zinazoathiri dunia na maadhimisho ya miaka 25, tangu kuanzishwa kwa mkutano wa kimataifa kuhusu wanawake.

Swala la uungwaji mkono azma ya kuangamiza silaha za kiniuklia pia litajadiliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *