Rais Kenyatta aongoza mazungumzo kati ya wajumbe wa Kenya na wa Somaliland

Rais Uhuru Kenyatta ameongoza mazungumzo kati ya wajumbe wa Kenya na wale wa eneo la Somaliland katika Ikulu ya Nairobi.

Wakiongozwa na Rais wao Musa Bihi Abdi, wajumbe wa Somaliland waliwasili Jumapili alasiri na kulakiwa na Waziri wa Kilimo Peter Munya na Katibu Mkuu Mwandamizi katika Wizara ya Mashauri ya Nchi za Kigeni Ababu Namwamba.

Kulingana na Msemaji wa Ikulu Kanze Dena Mararo, viongozi hao wamefanya mazungumzo kuhusu ajenda kadhaa zinazohusu ushirikiano kati ya Kenya na Somaliland.

Kikao chengine kama hicho kitaandaliwa Jumanne kwa ajili ya mazungumzo zaidi, huku Rais Abdi akitarajiwa kukamilisha ziara yake humu nchini katika muda wa siku tatu.

Somaliland ni mshirika muhimu katika eneo la upembe wa Afrika katika vita dhidi ya ugaidi na hasa kundi la Al-Shabaab.

Hii ni ziara ya pili ya kiongozi huyo wa Somaliland baada ya ziara sawa na hiyo ya Rais Kahin Riyale Kahin mwaka wa 2009.

Abdi aliapishwa tarehe 13 Desemba mwaka wa 2017 kama rais wa tano wa Somaliland.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *