Rais Kenyatta amuomboleza Askofu David Nguli Kalua

Rais Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa faraja kwa familia, jamaa na marafiki wa Askofu David Nguli Kalua aliyeaga dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 83.

Askofu huyo aliyeaga dunia alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali moja Jijini Nairobi ni babake Dkt. Isaac Kalua, mwanzilishi wa Wakfu wa Green Africa na pia Mwenyekiti wa Kampuni ya Honda Kenya.

Kwenye rambirambi zake, Rais Kenyatta amemtaja Askofu Kalua kama mtumishi wa Mungu halisi, ambaye mbali na kuhudumu kama kama mwenezaji wa injili, alitia bidii katika kuikuza familia yake vyema.

“Askofu David Kalua alikuwa mtu imara, mbali na mwito wake kama mtumishi wa Mungu, alijitahidi kufanya kazi ya mikono ili kujipatika kipato. Pia alikuwa mpenda elimu na alifanya juhudi za kusaidia wanafunzi werevu kutoka familia maskini wapate elimu,” amesema Rais.

“Askofu mwendazake pia alikuwa Mkenya Mzalendo aliyewachochea wale aliokutana nao kuipenda nchi yao na kufanya juhudi za kuifanya Kenya nchi nzuri kwa ajili ya wote,” akaongeza.

Kiongozi wa Taifa ameiombea Mungu familia hiyo ili ipate nguvu za kustahimili majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *