Rais Kenyatta amuomboleza aliyekuwa mkuu wa mkoa John Etemesi

Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala ya rambi rambi kwa familia, jamaa na marafiki wa John Khabeko Etemesi aliyefariki siku chache zilizopita.

Marehemu Etemesi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 90 alikuwa mkuu wa mkoa wakati wa enzi ya utawala wa hayati rais Daniel arap Moi.

Kwenye rambi rambi yake, Rais Kenyatta alimtaja Etemesi kuwa mkenya mtiifu na mzalendo aliyejitolea kulitumikia taifa hili kwa ukakamavu.

Rais alimtaja Mzee Etemesi kuwa mtu mnyenyekevu na mtumishi wa umma mwenye bidii aliyeacha kumbu kumbu katika maeneo yote ya nchi ambako alihudumu.

Aidha rais aliongeza kuwa Mzee Etemesi alikuwa afisa wa utawala aliyewakuza wengi katika utumishi wa umma.

Rais alimuomba Maulana kuipa nguvu familia ya mzee Etemesi wakati huu mgumu wa majonzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *