Rais Kenyatta ampongeza Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern kwa kuchaguliwa tena

Rais Uhuru Kenyatta amemtumia risala za pongezi Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern, kufuatia kuchaguliwa kwake tena kuhudumu kwa muhula wa pili.

Chama cha Leba cha waziri Adern kilishindi uchaguzi huo kwa wingi wa kura wa kihistoria na kupata viti 64 bungeni.

Kwenye risala yake ya kheri njema, Rais Kenyatta alimtakia Waziri Mkuu Ardern afya njema na ufanisi anapoongoza taifa lake kuafikia upeo mkubwa zaidi wa ufanisi.

Kenyatta pia ameahidi kwamba nchi hii itaendelea kushirikiana na New Zealand kama mshirika muhimu wa kimataifa.

Ardern alishinda hatamu ya pili uongozini jana na kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi kwa chama chake cha Leba katika muda wa nusu karne.

Wapiga kura walimzawadia kwa uongozi wake mwema ikiwemo jinsi alivyoshughulikia vyema janga la COVID-19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *