Rais Kenyatta akutana na wazee wa jamii ya Wasomali kutoka Garissa

Rais Uhuru Kenyatta leo amekutana na wazee wa jamii ya Wasomali kutoka Kaunti ya Garissa ambao walimtembelea katika Ukulu ya Nairobi.

Kiongozi wa Taifa na wazee hao wamejadili maswala mbali mbali ya kitaifa, ikiwemo miradi ya maendeleo katika eneo hilo.

Kwenye mkutano huo, ambao pia ulihudhuriwa na Mkuu wa Utumishi wa Umma Dkt. Joseph Kinyua, Waziri wa Fedha Ukur Yatani na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji, Rais Kenyatta alitambulishwa kwa Seneta mpya wa Kaunti ya Garissa Abdulkadir Haji.

Haji aliidhinishwa kama mgombea wa pekee na viongozi, wazee na wataalamu wa kijamii kutoka Kaunti hiyo kwa heshima ya marehemu babake aliyekuwa Seneta Yusuf Haji.

Wazee hao walikuwa wameandamana na Naibu Gavana wa Kaunti ya Garissa Abdi Dagane, Seneta wa Isiolo Fatuma Dullo, Wabunge Adan Keynan (Eldas), Aden Duale (Garissa Mjini), Sophia Abdi (Ijara) na Abdikarim Osman (Fafi), miongoni mwa viongozi wengineo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *