Rais Kenyatta ahudhuria ibada ya ukumbusho wa Marehemu Rais Mstaafu Moi

Rais Uhuru Kenyata ni miongoni mwa watu mashuhuri wanaohudhuria ibada ya ukumbusho wa Rais Mstaafu Daniel Arap Moi katika eneo la Kabarak, Kaunti ya Nakuru.

Moi aliaga dunia tarehe 4 mwezi Februari mwaka wa 2020, na hivi leo familia yake inaandaa ibada ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu afariki.

Rais Kenyatta ameugana na familia na marafiki kwa ibada hiyo ya ukumbusho inayoendelea nyumbani kwa marehemu Moi.

Rais pamoja na familia ya marehemu Moi wameweka shada za maua kwenye kaburi la marehemu rais mstaafu.

Viongozi wengine wanaohudhuria ibada hiyo ni pamoja na kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi, kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, Moses Wetangula wa Ford Kenya, miongoni mwa viongozi wengine.

Marehemu Rais Mstaafu Moi aliiongoza Kenya kwa miaka 24 kabla ya kustaafu mwaka wa 2002.

Aliaga dunia alipokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Nairobi, aakiwa na umri wa miaka 95.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *