Rais Kenyatta afanya ziara rasmi nchini Ufaransa

Rais  Uhuru Kenyatta alianza ziara  rasmi  nchini  Ufaransa Jumatano jioni  kwenye   Ikulu  ya    Elysee,    ambapo alikaribishwa  na  mwenyeji wake, Rais wa  Ufaransa, Emmanuel Macron.  

Baada ya kuwasili  muda mfupi baada ya  saa tatu  jioni, Rais  alikagaua gwaride la  lililoandaliwa na  wanajeshi wa Ufaransa  mnamo mwanzoni mwa sherehe ya kufana  ya kitaifa ya  makarabisho.

Viongozi hao hatimaye  walishuhudia   kutiwa saini kwa  mikataba kati ya    mataifa  haya mawili  kabla ya kuongoza jumbe zao kwenye  difa  iliyoandaliwa kwa heshima  ya Rais  Kenyatta.

Hatimaye viongozi hao walielekea kwa mashauriano ya    faragha.

Miongoni mwa  mikataba  iliyoafikiwa ni  mpango wa ufadhili wa serikali na  sekta  ya kibnafasi wa ujenzi wa  barabara kuu ya Nairobi-Nakuru-Mau, ulioatiwa saini kati ya   halmashauri ya Barabara Kuu Nchini na  kampuni ya Vinci Concessions.

Miradi mingine ni ujenzi wa reli  kutoka katikati  ya  jiji la Nairobi hadi  uwanja wa  ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na  mkataba wa utekelezaji wa mpango wa usambazaji wa umeme wa kiwango cha Kilo Watt 400 kutoka Menengai hadi Rongai.

Rais  atatoa hotuba muhimu  Alhamisi kwenye kongamano la kibiashara la mwaka huu la  BPI France Inno Generation

Ijumaa Rais ataongoza mkutano wa wafanyabiashara wa humu nchini na wenzao wa Ufaransa  ambao  unaandaliwa na   shirikisho la   wafanyabiashara nchini Ufaransa. 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *