Rais Kenyatta aagiza ujenzi wa Nyandika Mayioro Sports Academy huko Nyanturago

Rais Uhuru Kenyatta ameagiza  wizara ya michezo  kujenga  akademia ya michezo katika uwanja wa   Nyanturago  kaunti ya Kisii na kupewa jina la  Nyandika Mayioro Sports Academy.

Rais Kenyatta alisema haya Jumatatu alipohudhuria mazishi ya waziri wa zamani wa fedha  Simeon Nyachae  katika kaunti ya Kisii ambapo alitangaza kubadilishwa kwa jina uwanja wa Gusii kutoka Nyandika Mayioro hadi Simeon Nyachae kama njia ya kumuenzi na kumkumbuka  marehemu.

Mayioro alikuwa mwanamichezo wa kwanza kutoka kaunti ya Kisii akiwa Mkenya wa kwanza kushiriki michezo ya Jumuiya ya madola mwaka 1954.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *