Raila Odinga amhimiza naibu Rais William Ruto kujiuzulu

Kinara wa chama cha ODM  Raila Odinga amedai kuwa tofauti kati ya naibu wa rais  William Ruto na Rais Uhuru Kenyatta zimeathiri utekelezaji wa ajenda ya chama cha jubilee. 

Raila kwa mara ya kwanza alitoa wito kwa naibu wa rais William Ruto kujiuzulu iwapo anahisi kuwa hakuna uhusiano mwema kati yake na rais.

Raila alikuwa akiongea alipokuwa mwenyeji wa viongozi wapatao 600 wa kisiasa na mashinani kutoka jamii ya wakikuyu nyumbani kwa baba yake huko Bondo.

Raila alisema kuwa anataka kubuniwa kwa mfumo wa muda mrefu utakaowezesha  kupanuliwa kwa rasilmali za taifa hili kwa manufaa ya wakenya wote.

Raila aliukumbusha ujumbe huo kutoka eneo la Mlima Kenya juu ya uhusiano wa ki-historia kati ya jamii za Kikuyu na Luo na jinsi Marehemu Babake Jaramogi Oginga Odinga aliposhinikiza kuachiliwa kwa Jomo Kenyatta kutoka kizuizini.

Mkutano huo ulihudhuriwa na magavana watano kutoka eneo la  luo nyanza na naibu kiongozi wa chama cha  ODM Wycliffe Oparanya miongoni mwa viongozi wengine waliochaguliwa.

Baraza la wazee wa jamii ya wakikuyu liliongozwa na wabunge Jeremiah Kioni, Maina Kamanda na aliyekuwa mbunge wa  Gatanga Peter Kenneth, katibu mwandamizi  Zack Kinuthia pamoja na viongozi wengine waliochaguliwa.

Ujumbe kutoka eneo la Nyanza unatarajiwa kuzuru eneo la Mlima Kenya baadaye mwezi huu.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *