Raila awaonya Wakenya dhidi ya ‘kuhadaiwa tena na Ruto’

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga amewatahadharisha Wakenya dhidi ya kile alichokitaja kuwa kuhadaiwa kwa mara ya pili na Naibu Rais William Ruto na wandani wake.

Raila amesema kabla ya kuchaguliwa kwake, Ruto aliwahidi Wakenya mambo mengi, ila serikali anayohudumu haijafanikiwa kutimiza ahadi hizo.

Raila anashangazwa na jinsi Naibu Rais anazidi kuwapa Wakenya ahadi za endapo atachaguliwa kuwa rais mwaka wa 2022, ilhali hajatekeleza ahadi alizotoa awali kabla ya kuwa naibu rais.

Kiongozi huyo wa ODM amesema hayo baada ya kuhudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa moja la Katoliki katika mtaa wa Soweto, Eneo Bunge la Embakasi, ambako amewarai waumini kuunga mkono mchakato wa BBI.

Raila amesema maslahi ya makanisa yamenakiliwa vizuri kwenye ripoti ya BBI, baada ya mashauriano ya kina baina ya wana kamati wa BBI na wawakilishi wa makanisa.

Aidha, Raila amewashtumu wanaopinga ripoti hiyo, akiwataja kuwa wanafiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *