Raila asimikwa mzee wa jamii ya Waduruma

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amesimkwa kuwa Mzee wa Jamii ya Waduruma ,kwenye hafla iliyoandaliwa katika sehemu ya Samburu,kaunti ndogo ya Kinango,kuanti ya Kwale.

Waziri mkuu huyo wa zamani ambaye yuko katika ziara ya kupigia debe mchakato wa BBI,alipewa jina Mzee Mgandi,lenye maana mti mkubwa katika utamaduni wa jamii hiyo.

Odinga alitoa wito kwa wakazi wa eneo la Pwani kuunga mkono marekebisho ya katiba kupitia BBI,akisema marekebisho hayo yanaangazia utatuzi wa swala la umiliki wa ardhi na uimarishaji uchumi wa shughuli za baharini,miongoni mwa manufaa mengine.

Aidha alisema BBI inapendekeza kuongezwa kwa mgao wa serikali za kaunti,hatua alisema itaiwezesha kaunti hiyo kutekeleza kwa urahisi miradi yake ya maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *