Raila asema BBI ndio suluhisho kwa changamoto za kihistoria

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesisitiza kuwa mchakato wa BBI ndio sulushisho kwa changamoto zinazolikabili taifa hili tangu uhuru.

Kulingana na Raila, mchakato wa BBI ambao utaashiria kura ya maamuizi kuhusu marekebisho ya katiba utahakikisha ushirikishwaji wa Wakenya wote na uwajibikaji serikalini.

Kinara huyo wa chama cha ODM amesema marekebisho yaliyopendekezwa chini ya mchakato wa BBI yatahakikisha usawa wa kijinsia na ujumuishwaji wa vijana katika maamuzi.

Raila amesema hayo alipohutubia zaidi ya vijana 800 katika jumba la ufungamano kabla ya kuanza kwa shughuli ya uhamasisho kuhusu ripoti ya BBI ambayo itang’oa nanga hivi karibuni.

“Tunayopendekeza ni suluhisho kwa matatizo yaliyopo na tunataka Wakenya waelewe vizuri ili wananchi waweze kupitisha bila kupingwa. Yote tunayofanya leo ni kwa manufaa ya watoto wa vijana wa taifa hili,” amesema Raila.

Kwa mara nyingine, Raila ameunga mkono matamshi ya Rais Uhuru Kenyatta wakati wa mazishi ya mamake kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi kuwa urais uwe ukizunguka kwa jamii zote.

Raila amesema matamshi hayo yalitolewa wakati mwafaka, ikitiliwa maani mchakato wa BBI na malengo yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *